manyaki-1.jpg ...      ...

SIMBACHAWENE:WALIOKULA PESA ZA TASAF WAZIREJESHE MAPEMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.* *Mhe. Simbachawene pia amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwasimamisha kazi Waratibu wote wa TASAF wilaya ili kufanya uchunguzi wa jinsi walivyojihusisha katika kuvuruga utekelezaji.
Simbachawene amesema pia wote watakao patikana na hatia wafikishwe katika vyombo vya dola.
Na kuwaagiza wakurugenzi wafatilie kwa karibu watendaji na wenyeviti Wa vijiji pamoja na maafisa tasaf ambao sio waaminifu.
Huku simbachawene akitaja mikoa kama dar,mbeya,Arusha na Kilimanjaro kuwa NI waanga Wa janga hilo LA utapeli Wa pesa za Tasaf.
Previous
Next Post »