manyaki-1.jpg ...      ...

MWIGULU NCHEMBA ATOA ONYO KALI KWA MADEREVA WA MAGARI.

Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (mb), ameliagiza jeshi la polisi nchini,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.
Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida, ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha 38 cha bodi ya barabara mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.
Amesema baadhi ya madereva wa magari na hasa yale makubwa,hutumia mawe kuzuia magari yao kutembea wakati wakiyafanyia matengenezo
Amedai kuwa wakishamaliza shida zao,uyaacha matawi Barabarani ambapo matawi na mawe  yanaweza leta madhara kwa watumiaji Wa barabara.



Previous
Next Post »