manyaki-1.jpg ...      ...

WAZIRI JANUARY MAKAMBA UZULU KILOSA KUTATUA MIGOGORO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba amekutana na kuzungumza na wakazi wa kijiji cha Mbwade, Kata ya Madoto, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa jamii.
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-23-am
Waziri Makamba akiwa na viongozi wa wilaya na mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoi, ambaye amesikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa kijiji hicho ambacho kinakaliwa na wakulima na wafugaji ambapo kwa kiasi kikubwa wameeleza changamoto kubwa ya mgawanyo bora wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji hasa katika kipindi cha ukame kuanzia mwezi wa 9, 10 na 11 ambacho kimetajwa kuwa na migogoro sana.
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-24-am
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-25-am
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-26-am
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-27-am
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-28-am
whatsapp-image-2016-10-17-at-9-45-30-amPICHA ZOTE HAPO JUU ZIKIMUONYESHA WAZIRI MAKAMBA ALIPOZURU SEHEMU ZENYE MIGOGORO
Katika kushughulikia changamoto za mikwaruzano kati ya wakulima na wafugaji Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa kamati jumuishi ya amani ya kijiji ambapo ameahidi kuhakikisha kamati hiyo inapata mafunzo maalum ya upatanishi wa migogoro inayohusiana na rasilimali huku pia akiagiza kuundwa kwa kamati za mazingira kila kijiji na kata ambayo pia itapatiwa mafunzo maalum ya utunzaji wa mazingira hasa katika maeneo yenye ukame.
Katika ziara hiyo, Waziri Makamba alifika katika kijiji cha Twatwatwa kata ya Parakuyo na kujionea changamoto wanazokumbana nazo wafugaji hasa kipindi cha kiangazi na kuwaasa wananchi hao kushiriki katika zoezi la uhakiki wa mifugo ili kuirahisishia kuweka mipango sahihi ya kuwasaidia, huku akisisitiza juu ya matumizi bora ya ardhi kwa wakulima na wafugaji
.
Previous
Next Post »