Mheshimiwa Sitta akisimikwa kuwa Mjukuu Mkuu wa ukoo wa Fundikira katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Unyanyembe Itetemia mkoani Tabora jana.
Mheshimiwa Samweli Sitta akitangaza nia mbele ya umati wa wananchi katika uwanja wa Ikulu ya Unyanyembe katika manispaa ya Tabora.
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii, Tabora.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa anataka Urais wa miaka mitano kuweza kuivusha nchi katika kutokana na mambo yanayoonekana ikiwamo muungano,udini ,ungezeko la vijana.
Sitta ameyasema hayo leo wakati akitangaza nia ya kugombea urais katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chifu Fundikira Kata ya Itetemia mkoani Tabora.
Amesema mtu yeyote makini ana nafasi ya Urais, hana budi kuyapima mazingira ya taifa katika miaka mitano ijayo na kuzielewa changamoto zitakazokuwepo katika kipindi cha uongozi anachokusudia kuongoza.