Ilikuwa 23/11/2016 jumatano jana ndani ya kipindi cha XXL ya Clouds FM ambapo mkali wa Bongo Fleva Diamond Platnumz alikuwa na exclusive interview katika kipindi hicho akiitambulisha ngoma yao mpya ambayo amefanya na Rich Mavoko inayoitwa Kokoro.
Interview hiyo ilimake headlines kinoma noma kutokana na Diamond Platnumz kufunguka moja kwa moja bila kuficha ficha kuhusu tofauti za yeye na wasanii wenzake Alikiba na Ommy Dimpoz.
Moja kati ya points kibao ambazo zilizungumzwa jana na mkali huyo hapo jana ni hii hapa ambayo nimeamua kukusogezea kwa muda huu kuhusu wakali hao wenye upinzani mkubwa kuonyesha ukali wao kwenye collabo.
“Kama wewe unajua una fact, njoo studio tufanye kazi. Hao watu wanaosema ni wakali nimesha waomba collabo tufanye wamenikimbia, hao watu wanaosema ni wakali nimesha waomba show tufanye mkali nani wakanikimbia, kama wao wanajiona ni wakali kwanini wananikimbia!?”Alisema Diamond Platnumz.
Play hii video hapa chini kumsikiliza Diamondakifunguka mengi juu ya issue hiyo.
- Diamond ajibu vijembe vya Ommy Dimpoz kuhusu muziki wa ujanja ujanja na mengineyo!