Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama
chake cha CUF kimebaini uwepo wa mpango mahsusi unaoratibiwa na Tume ya
Uchaguzi Zanzibar – ZEC, wa kupandikiza watu wasio na sifa pamoja na
wapiga kura hewa kwa ajili ya kukipa ushindi chama tawala CCM katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari jijini Dar es Salaam, maalim Seif amesema mpango huo unahusisha mbinu kadhaa chafu ikiwemo ya kuwaandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, vijana ambao hawajatimiza umri pamoja na watu kujiandikisha zaidi ya mara moja na katika maeneo yasiyokuwa ya kwao.

Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mbinu nyingine
ni ya kuwatumia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, ambao
hivi sasa wamekuwa wakihamishiwa katika kambi ya jeshi ya Chukwani
kisiwani Zanzibar, kitendo alichodai kuwa ni hatari kwani kitaharibu
kabisa matokeo na taswira ya uchaguzi mkuu ujao.