17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi''
17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''17:05 Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huru
17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.
16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais Nkurunzinza
16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.
16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.
16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi.
16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi
16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari''
16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura
15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.
15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.
15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.
15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.
15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.
Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''
WANANCHI WA BURUNDI WAKISHANGILIA BAADA YA RAIS WAO KUN'GOLEWA MADARAKANI.
