manyaki-1.jpg ...      ...

Mali ya uma yamtia mashakani waziri mkuu wa ufaransa.

Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, amesema amejutia kitendo chake cha kutumia ndege ya serikali kupeleka wanawe kutizama fainali ya mechi ya mabingwa wa ligi kuu barani Ulaya Jumamosi iliyopita mjini Berlin.
Bwana Valls alijikuta matatani baada ya kutumia ndege hiyo akiandamana na wanawe wawili kutizama fainali hiyo kati ya Barcelona na Juventus.
Hata hivyo amesizitiza kuwa yeye binafsi alikuwa kazini kuhudhuria mkutano aliyoalikwa na rais wa UEFA, Michel Platini, ili kujadili mashindano ya Euro ya mwaka 2016 championship, ambayo Ufaransa ndio mwenyeji.
Lakini sasa amesema atalipa dola 2800 zilizotumika kwa wanawe hao wawili na kwamba hatarudia tena kitendo hicho.
Previous
Next Post »