Waziri
mkuu wa Australia, Tony Abbott, ameyaomba mataifa ya Asia-Pacific
kuungana ili kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi.
Abbot amewaambia mawaziri kutoka kwa mataifa 25 katika mkutano wa kikanda unaofanyika mjini Sydney kuhusu usalama.
Amesema
kuwa kundi la Islamic State lina nia ya kutawala dunia, huku akielezea
kuwa hilo ni kundi la mauti, lenye mafunzo mabaya ya itikadi kali.
Waziri huyo mkuu ameongeza kuwa Australia imeamua kuzuia raia wa nchi hiyo kujiunga na wanamgambo wa Islamic State
wapiganaji wa islamic state
Amesema hayo muda mfupi baada ya Rais Barrack Obama kuidhinisha wakufunzi 450 wa jeshi la Marekani, kwenda Iraq.
White
House sasa inasema kuwa ina imani mikakati yake ya kutoa mafunzo kwa
vikosi vya kiusalama vya Iraq na kuwaingiza jeshini wapiganaji wa
kikabila wa Sunni, itafaulu katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa
Islamic State.