Rais Obama
Rais Obama katika ziara yake ya
kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba
linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora.
Akizungumza
katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya
mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na
kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika.Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.
Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yalioafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo.
http://frankmanyaki.blogspot.com/