Shirika
moja la kujtetea haki limeihsutumu mojawepo ya kampuni kubwa zaidi
duniani ya mauzo ya mawese, iliyoko nchini Liberia, kwa kutumia mlipuko
wa ugonjwa wa Ebola kujitajirisha.
Shirika hilo, Global Witness,
limesema kuwa wakati mlipuko huo ulipokuwa kilele Afrika Magharibi mwaka
uliopita, kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari kwa
maandalizi ya upanzi wa mmea huo wakati ambapo makundi ya missada kwa
jamii yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na
ugonjwa huo.Hata hivyo kampuni hiyo imejibu katika barua walioandika kwa shirika hilo la Global Witness kuwa kandarasi ya pekee waliosaini mwaka huo, ilitokana na kazi zao za miezi au hata miaka kabla ya kuzuka ugonjwa huo.
Wanaharakati wa mazingira
wamekuwa wakilaumu wakulima wa mashamba makubwa ya mawese kwa uharibifu
wa mazinginra na ongezeko la joto duniani.
http://frankmanyaki.blogspot.com/
http://frankmanyaki.blogspot.com/