manyaki-1.jpg ...      ...

DIAMOND PLATNUMZ PAMOJA NA WASAFII KUJA NA PLATFORM YA KUUZA NYIMBO ONLINE

Wiki iliyopita msanii Diamond Platnumz alifanya interview na kipindi cha Jahazi cha Clouds fm.
Na moja kati ya mambo ambayo aliyazungumza mkali huyo ni pamoja na jinsi gani amejipanga kuondoa kero za upakuaji wa nyimbo katika mitandao.
Kitu ambacho alidai kuwa kinawakera wengi kutokana na kuwa na process ndefu kama kujisajili na vitu kama hivyo endapo mtu atahitaji kupakua wimbo na hivyo kumfanya mtu kupata shida wakati wa kupakua wimbo.
Diamond aliweka wazi mipango yake na team yake nzima kuwa wanajipanga kabla ya mwaka huu kuisha kuhakikisha wamewaletea mashabiki wao Platform ambayo itawawezesha kupata kazi zao kwa urahisi bila usumbufu kama ilivyo sasa.
“Kabla ya huu mwaka kuisha tutakuwa tuna App yetu sisi wenyewe na Platform au website ambayo zitapatikana nyimbo za Wasafi zote kiurahisi na bila kuwa na mlolongo mrefu. Tumeamu kufanya hivyo kwa kutambua kuwa watu wanatamani kupata nyimbo zetu lakini wanazipata kwa tabu sana. Na hivi sasa Platform hiyo iko inamaliziwa na pia tupo katika maongezi tu na baadhi ya makampuni kwasababu kuna baadhi ya kazi ambazo zitakuwa zinachajiwa kwa gharama ndogo tu kama Tsh. 50 au 100 tu mtu aweze kupata nyimbo.” Alisema Diamond Platnumz.

Previous
Next Post »