manyaki-1.jpg ...      ...

NDEGE YA MAKAMU WA BWANA TRUMP YAPATA AJALI

                        Picha ya Ndege aliyopanda mgombea mwenza wa trump ikiwa imepaki   kwenye nyasi baada ya kupata dhoruba hilo.
Mgombea mwenza wa chama cha Republican katika kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani Mike Pence amenusurika baada ya ndege iliyombeba kuteleza uwanja wa ndege.
Ndege hiyo iliteleza na kuvuka barabara inayotumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja wa LaGuardia jijini New York.
Gavana huyo wa Indiana amewaambia wanahabari kwamba yuko salama baada ya kisa hicho.
Hakuna aliyejeruhiwa.
Bw Pence na abiria wengine takriban 30 waliokolewa kupitia mlango wa dharura wa ndege upande wa nyuma.
Alikuwa anatoka mkutano wa kampeni Fort Dodge, Iowa.
Uwanja wa ndege wa LaGuardia kwa muda usiojulikana, maafisa wamesema.
Rubani anadaiwa kukanyaga breki na abiria wanasema walinusa harufu ya raba ikiungua.
Kanda za video za runinga zimemuonesha Bw Pence baadaye akiwa amesimama kwenye mvua karbu na magari ya huduma za dharura, akizungumza na baadhi ya maafisa.
Baadaye aliandika kwenye Twitter: "Nashukuru sana kwamba kila mtu aliyekuwa kwenye ndege yetu yuko salama. Nashukuru maafisa wa dharura na wote waliotuombea. Tutarejea kwenye kampeni kesho!"
Clinton tweetImage copyrightTWITTER
Amesema matope yaliruka na kujaa kwenye kioo cha sehemu ya mbele ya ndege.

Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump alimpigia simu Bw Pence kumjulia hali baada ya kisa hicho, maafisa wa kampeni wamesema.
mike pence akitoka ndani ya ndege iliyombeba baada ya kupata dhalula
Previous
Next Post »