manyaki-1.jpg ...      ...

KIJANA MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI ALIYETEMBEA NA WANAWAKE 104 AENDA JELA MIAKA MIWILI

Mahakama nchini Malawi imemhukumu  miaka miwili kwenda jela kijana erick avina mwenye virusi vya HIV ambaye alikiri kufanya tendo la ngono na zaidi ya wanawake 100 na wasichana bila kutangaza hali yake.
Katika uamuzi mkubwa uliotarajiwa na wengi,Eric Aniva alipatikana na hatia ya ''kutekeleza mila zenye madhara'' chini ya sheria za kijinsia za taifa hilo baada ya uchunguzi  kubaini vile alivyolipwa ili kuwafanyia sherehe za kutakasa wasichana wadogo pamoja na wanawake wajane.
Eric Aniva ni mwanamume wa kwanza kufungwa jela kuwa 'fisi' neno linalotumika kwa mwanamume anayelipwa ili kushiriki ngono na wanawake pamoja na wasichana ikiwa ni miongoni mwa tamaduni za kutakasa.
Katika mahojiano yake na mwandishi Wa habari,alikiri kufanya mapenzi na wanawake 104 na wasichana bila kuwalezea kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya HIV.
Ijapokuwa hakuna msichana aliyejitokeza, kulalamika, alipatikana na hatia ya kutekeleza mila zenye madhara baada ya wanawake wawili kutoa ushahidi wao.
Wote wawili ni wajane ambao wanasema walilazimishwa kufanya mapenzi na mtu huyo ili kutakasa roho za waume zao baada ya vifo vyao.
Kesi hiyo imezua maoni tofauti nchini Malawi huku baadhi yao wakidai kwamba sheria kali za kijinsia zinaingilia utamaduni na kwamba bw Aniva anasulubiwa .
Wakati huohuo mashirika ya haki za kibinaadamu yanaamini kwamba kesi hiyo ni ushindi katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kingono.
Previous
Next Post »