manyaki-1.jpg ...      ...

RAIS MAGUFULI ASHINDWA KUFURUKUTA KWA THULI MADONSELA

Thuli Madonsela
Bi Madonsela aliwashinda marais watatu wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wa nchi ya Rwanda katika kushinda tuzo hiyo.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec.
Bi Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa Nairobi Alhamisi jioni, amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini. Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita.
Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani.
Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011. Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipo fanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta.
Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.
Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili. Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
WASHINDI WA AWALI NI:
■2011 – Sanusi Lamido Sanusi, aliyekuwa wakati huo Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria.
■2012 – James Mwangi, CEO wa Benki ya Equity, Kenya
■2013 – Akinwumi Adesina, aliyekuwa wakati
huo Waziri wa Kilimo Nigeria.
■2014 – Aliko Dangote, mwenyekiti wa CEO wa kampuni ya Dangote Group, Nigeria.
■2015 – Mohammed Dewji, CEO wa kampuni ya
MeTL Group, Tanzania

Previous
Next Post »