manyaki-1.jpg ...      ...

SPIKA WA BUNGE MSTAAFU MH SAMWEL SITA AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa spika Wa bunge la jamhuri wa muungano wa tanzania katika serikali ya awamu ya nne mh ndugu samwel Sitta amefariki dunia nchini ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.
habari toka kwa mmoja wa watoto wa familia bwana ben sitta ambaye pia ni meya wa kinodoni amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake.
habari zinasema kuwa mh Sitta alikuwa amelazwa katika hospitali nchini ujerumani toka mwezi jana alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tenzi dume,ambapo inasemekana kuwa ugonjwa huo ulikuwa umeshamuathiri sehemu kubwa ya viungo vya mwili wake ikiwemo miguu na kumkwamisha kutembea.
watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa spika wa bunge wa sasa  ndugu job ndugai na kwa familia akiwemo rais magufuli.

Previous
Next Post »