manyaki-1.jpg ...      ...

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AGUNDUA MADUDU YA ZEC KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama chake cha CUF kimebaini uwepo wa mpango mahsusi unaoratibiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar – ZEC, wa kupandikiza watu wasio na sifa pamoja na wapiga kura hewa kwa ajili ya kukipa ushindi chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari jijini Dar es Salaam, maalim Seif amesema mpango huo unahusisha mbinu kadhaa chafu ikiwemo ya kuwaandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, vijana ambao hawajatimiza umri pamoja na watu kujiandikisha zaidi ya mara moja na katika maeneo yasiyokuwa ya kwao.
Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mbinu nyingine ni ya kuwatumia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, ambao hivi sasa wamekuwa wakihamishiwa katika kambi ya jeshi ya Chukwani kisiwani Zanzibar, kitendo alichodai kuwa ni hatari kwani kitaharibu kabisa matokeo na taswira ya uchaguzi mkuu ujao.
Previous
Next Post »