Mwanasiasa wa chama cha Republican,
na gavana wa jimbo la Florida, Jeb Bush ametangaza rasmi ametangaza
rasmi nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa taifa hilo kubwa duniani
kiuchumi kwa tiketi ya chama hicho cha Republican.
Akizungumza
katika mkutano wake wa hadhara huko Miami,Jeb ambaye baba yake na kaka
yake wamewahi kuongoza Marekani ameubeza utawala wa Rais Obama katika
sera zake za mambo ya nje.Lakini mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini anasema Jeb Bush pia anaweza kutegemea mtandao wa kisiasa wa kifamilia na nguvu ya uchangishaji.