Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel
Valls, amesema amejutia kitendo chake cha kutumia ndege ya serikali
kupeleka wanawe kutizama fainali ya mechi ya mabingwa wa ligi kuu barani
Ulaya Jumamosi iliyopita mjini Berlin.
Bwana Valls alijikuta
matatani baada ya kutumia ndege hiyo akiandamana na wanawe wawili
kutizama fainali hiyo kati ya Barcelona na Juventus.Hata hivyo amesizitiza kuwa yeye binafsi alikuwa kazini kuhudhuria mkutano aliyoalikwa na rais wa UEFA, Michel Platini, ili kujadili mashindano ya Euro ya mwaka 2016 championship, ambayo Ufaransa ndio mwenyeji.
Lakini sasa amesema atalipa dola 2800 zilizotumika kwa wanawe hao wawili na kwamba hatarudia tena kitendo hicho.