manyaki-1.jpg ...      ...

YALIYOJIRI KATIKA MSIBA WA MTOTO WA NYERERE,JOHN NYERERE

Rais Kikwete aifariji familia ya Nyerere kufuatia kifo cha John Nyerere.

 

VIONGOZI MBALI MBALI WASHIRIKI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MTOTO WA BABA WA TAIFA JOHN NYERERE.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa 

marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. 
Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria 
Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani 
kwao Butiama. Picha na OMR
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu John Nyerere.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha rambi rambi kwenye msiba wa John Nyerere
 Makama Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye msiba wa John Nyerere .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kwenye msiba wa John Nyerere ambapo viongozi mbali mbali walijumuika kutoa heshima za mwisho.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonyesha jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)Philip Mangula kwenye msiba wa John Nyerere ,msasani jijini Dar es salaam.(Picha na Adam Mzee)
 Makongoro Nyerere akisoma wasifu wa Marehemu John Nyerere
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akisaini kitabu cha rambi rambi nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam ambapo alifika kumpa pole Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia msiba wa mtoto wa Baba wa Taifa John Nyerere.

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.
 Ndugu akitoa pole kwa Mama Maria Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa mkono wa pole Mama Maria Nyerere kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mama Maria Nyerere alipofika nyumbani kwake kumpa pole kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere, wengine pichani ni Makongoro Nyerere (kushoto), Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi, na Anna Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John Nyerere.

WASIFU WA MAREHEMU JOHN GUDDO NYERERE:
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda.
Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi. AMENI
 
Picha ya Marehemu John Nyerere aliyefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.


MTOTO WA MWALIMU NYERERE AZIKWA LEO BUTIAMA

 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akisali mbele ya jeneza la marehemu John Guido Nyerere kabla halijaingia kanisani kwa ajili ya ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.
 Viongozi na wananchi wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu John Gaudo Nyerere katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa ,Butiama.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Mtoto wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna Nyerere.
 Ni huzuni kwa kila mtu.
 Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Mtoto wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu John Gaudo Nyerere mara baada ya kuweka taji la maua.
 Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu John Nyerere kwenye mazishi yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Baba wa Taifa Butiama.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishiriki kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Baadhi ya Watoto wa marehemu pamoja na ndugu wengine.
 Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akisoma salaam za rambi rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wakati wa mazishi ya John Nyerere
 



 
Emily Magige Nyerere akifafanua jambo wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere.
 Mbunge wa Monduli na waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimfariji Mjane wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha mtoto wake John Nyerere wakati wa mazishi ya mtoto huyo wa nne wa Nyerere katika kijiji cha Mwitongo, Butiama, mkoani Mara leo.
Askari wa JKT wakiwa na mashada ya maua mbele ya jeneza lililo na mwili wa Mpiganaji Vita ya Kagera, Marehemu John Nyerere.
 Lowassa akisalaimana na wananchi wa Mwitongo.
 Lowassa akisaliama na mmoja wa viongozi wa dini mkoani Mara.
 Sehemu ya Viongozi wakiwa katika mazishi hayo leo.
 Viongozi wakiwa msibani hapo.
 Edward Lowassa (MB) akisaliama na baadhi ya wananchi wa Mwitongo, Butiama baada ya kushiriki mazishi ya John Nyerere leo.
 Mbunge wa Monduli akimfariji kaka wa Marehemu, madaraka Nyerere.
 

Previous
Next Post »