Umoja wa mataifa umesema mjumbe wake
maalum katika eneo la maziwa makuu hataendelea tena kuwa mpatanishi
katika mzozo wa Burundi.
Msemaji wa umoja huo Vladimir Monteiro
amesema mjumbe huyo Said Djinnit amejiondoa kutoka kwa harakati hiyo
iliyokuwa inatafuta mwafaka kati ya vyama vya upinzani na kile
kinachotawala cha rais Pierre Nkurunziza anayekabiliwa na shinikizo za
maandamano kila uchao kupinga hatua yake ya kuwania muhula mwengine kama
rais wa nchi hiyo.Hakuna sababu zozote zilizotolewa kuhusu kujiondoa kwa bwana Djinnit lakini awali makundi ya upinzani yalikuwa yamedai kuwa afisa huyo alikuwa anaupendelea upande wa serikali madai anayoyakana.
Licha ya hatua hiyo bwana Djinnit ataendelea kuwa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika nchi za maziwa makuu.