Mashambulizi ya mabomu huko Sanaa
Mfululizo wa milipuko ya mabomu
imeendelea kurushwa katika misikiti ya Shia na Ofisi zilizopo katika la
jimbo la Yemen, Sanaa, na kusababisha vifo vya watu 30.
Mashambulizi
hayo ya mabomu yamewalenga waumini wa Shia waliokuwa katika ibada yao
ya jioni, na Ofisi ambayo yanatumiwa na kikundi cha waasi wa Houthi.
Wanamgambo
wa Islamic State wamekiri kuhusika na milipuko hiyo na kudai kuwa ni
hatua yao ya kulipa kisasi dhidi ya Houthi, walioteka jimbo la Yemen na
milki zake.
Kwa sasa mazungumzo yanaendelea huko Geneva kati ya
waasi na Serikali,huku maofisa wa umoja wa mataifa wakijaribu
kusuluhisha pande hizo mbili ili kusitisha mapigano.
TUMA HABARI KWA NJIA YA WHATSAAP IWE YA LEO NA MATANGAZO YOTE KWA BEI RAHISI KUPITIA 0742418010