Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke
Askari
polisi mmoja wa kituo cha polisi Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa
Temeke, ameuawa kikatili siku ya ijumaa mchana baada ya kupigwa risasi
ya kifua na majambazi waliokuwa wanajaribu kutoroka baada ya kufanya
tukio la kihalifu. Askari hao waliokuwa doria katika eneo la Wailes
walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na majambazi hao mara baada ya
majambazi hao kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri
wa pikipiki kipindi ambapo askari polisi walikuwa karibu na eneo la
tukio. Hata hivyo wakati askari hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao
wawili kwa lengo la kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na
kumpiga risasi ya kifua askari huyo na kufariki pale pale.
Mwili wa askari huyo ukiwa umehifadhiwa.
Hata
hivyo katika harakati za kujaribu kukimbia majambazi hao walianguka na
pikipiki waliyokuwa wakitumia ndipo wakaamua kutimua mbio mitaani na
kuingia katika nyumba moja ambapo walijificha na kujifanya kama ni
wakazi wa eneo hilo, baada ya wnanchi na polisi kufika katika nyumba
hiyo, baadhi ya majirani waliwaambia polisi kwamba wameona watu hao
wameingia katika nyumba hiyo. Baada ya polisi kuingia waliwakuta watu
hao wakiwa wametulia kama kwamba wao ni wakaazi wa nyumba hiyo na wala
hawajui lililotokea.
Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti
Baada
ya kuwatambua watu hao, polisi waliwatia nguvuni huku wananchi wenye
ghadhabu waking'ang'ania kuwa wanataka kuwaua sababu wameshaua askari
mmoja. Baada ya vuta nikuvute kati ya wananchi na askari hao ambao
walikuwa wachache, wananchi walifanikiwa kuwachukua majambazi hao kwa
nguvu kutoka mikononi mwa polisi na kuanza kuwapiga kwa silaha
mbalimbali za kienyeji yakiwemo mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao
wakapoteza maisha.
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Mwili wa askari polisi ukiwa umepakiwa kwenye gari ya polisi tayari kupelekwa hospitali ya Temeke kuhifadhiwa.Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo waliiambia blogu hii kwamba majambazi hayo
kabla ya kupambana na polisi walikuwa wamefanya uvamizi na kumuibia
mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo. Hata hivyo mali au fedha iliyoibiwa
haikuweza kujulikana mara moja.
Askari polisi mmoja wa kituo cha polisi Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa Temeke, ameuawa kikatili siku ya ijumaa mchana baada ya kupigwa risasi ya kifua na majambazi waliokuwa wanajaribu kutoroka baada ya kufanya tukio la kihalifu. Askari hao waliokuwa doria katika eneo la Wailes walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na majambazi hao mara baada ya majambazi hao kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri wa pikipiki kipindi ambapo askari polisi walikuwa karibu na eneo la tukio. Hata hivyo wakati askari hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao wawili kwa lengo la kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na kumpiga risasi ya kifua askari huyo na kufariki pale pale.
Mwili wa askari huyo ukiwa umehifadhiwa.
Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti
Baada ya kuwatambua watu hao, polisi waliwatia nguvuni huku wananchi wenye ghadhabu waking'ang'ania kuwa wanataka kuwaua sababu wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta nikuvute kati ya wananchi na askari hao ambao walikuwa wachache, wananchi walifanikiwa kuwachukua majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi mwa polisi na kuanza kuwapiga kwa silaha mbalimbali za kienyeji yakiwemo mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao wakapoteza maisha.