Bila shaka umeshawahi kufikiria kuhusu mrithi wa mali zako siku ikitokea haupo duniani, japokuwa kwa tamaduni za kiafrika ni watu wachache sana huwa wanaweka wazi au kuandika taarifa kuhusu warithi wa mali zao pindi ikitokea wamefariki dunia.
Sasa leo nimeipata hii kuhusu atakayerithi mali au utajiri wa Bill Gates ambaye ni tajiri namba moja wa dunia kwasasa.
Kwa mujibu wake mwenyewe Gates amesema hataacha utajiri wake unaotajwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 81.7 kwa watoto wake watatu na badala yake atatoa kiasi dola za Marekani Bilioni 70 kwa watu wanaohitaji msaada dunia nzima, na tayari watoto wake wote wanajua kuhusu maamuzi yake na wamemuelewa.
Akizungumza kupitia kipindi cha Holly Willoughby na mtangazaji Ben Shephard, Mmiliki huyo wa kampuni ya Microsoft mwenye miaka 60 amesema “Ndio, watoto wetu wanapata elimu bora sana na tunawapa pesa za kutosha lakini kuna siku watakwenda kuanza maisha yao na kufanya kazi zao.” – Bill Gates
Bill Gates amesema kuwa endapo ataruhusu watoto wake wawili wakike na mmoja wa wa kiume warithi utajiri wake watakachokifanya ni kuzichezea tu pesa zake.
Mfanyabiashara huyo mkubwa amesema kuwa ana uhakika watoto wake hawawezi kuwa masikini na ameshawawekea uhakika wa maisha yao watakapoanza maisha yao siku za baadaye. Bill Gates na mkewe Mellinda mwenye miaka 52 wana watoto watatu ambao Jennifer mwenye miaka 20, Rory mwenye miaka 17, ana Phoebe mwenye miaka 14.