Mkongwe wa muziki wa Kizazi kipya Dully Sykes, amevitaka vyombo vya habari kumsapoti msanii mwenzie wa Kitambo Q Chillah kwa sababu anaamini bado anauwezo mkubwa zaidi kimuziki.
Dully ameiambia Times Fm kuwa, Q chillah ni msanii bora kwake na mwenye sauti ya pekee muda wote ila anachokosa kwa sasa ni sapoti kutoka kwenye Vyombo vya Habari.
MkaLi huyo wa Inde ametaka nguvu inayoelekezwa kwa wasanii wengine wanaofanya vizuri kwa sasa, imuangazie pia Q Chillah na huenda akarudi na nguvu zaidi.