Zaidi ya watu 50 wanaripotiwa kuuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka nje ya mji wa Malakal nchini Sudan Kusini.
Vikosi vya waasi viliendesha mashambulizi kwenye mji huo wa pili kwa ukubwa siku ya Ijumaa, baada ya kuteka vijiji vilivyo karibu.
Hata hivyo serikali inasema kuwa wanajeshi wake wamewatimua waasi hao hatua iliyosababisha maafa mengi.
Msemaji wa waasi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa wana matumaini ya kuteka mji wa Malakal na kuongeza kuwa hakuna matumaini ya kuwepo makubaliano kati ya kiongozi wao Riek Machar na rais Salva Kiir pamoja na kati ya kabila la Nuer na lile la Dinka.