Uhusiano wa Jokate na Alikiba una takriban miaka miwili sasa lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kukiri hadharani.
Waswahili husema penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Ndio maana pamoja na kujitahidi sana kuuficha, uzito wa penzi lao umekuwa ukiacha mianya mingi inayodhihirisha uwepo wake mbele ya hadhira.
Na sasa huenda Jokate akawa ameuweka wazi zaidi kwa salamu za birthday alizomtumia mpenzi wake huyo aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa, November 29.

Akijaribu kutomwaga mchele kwenye kuku wengi, Jojo ametumia lugha ya Kifaransa kuwasilisha ujumbe wake.
Shabiki mmoja anayeielewa lugha hiyo ametafsiri post yake kwa Kiingereza inayosema:
Baby happy birthday I love you so much,it is paining,I hope that the French has sang you prepare for that, but I want nothing,but the best for you from the bottom of my heart the rest I leave to God for what happens to know that Jojo doesn’t disturb and that am happy to have you as my friend,rest blessed