Kanye West amekuwa kwenye headlines mbali mbali wiki hii, na mojawapo ni hii ya kukatisha show aliyokuwa akiifanya huko Sacramentino California na kuanza kuwachana Beyonce na Jay Z kwenye steji kwa alichodai kwamba wamemkosea.
Baada ya kumaliza kuwachana Jigga na Bey Kanye alitupa Mic chini na kuondoka, kitu ambacho kililalamikiwa na mashabiki kwa sababu alikuwa ameperfom nyimbo tatu tu.
Waandaaji wa show hiyo wamewaahidi mashabiki kulipwa pesa zao ndani ya siku 5 mpaka 7 za kazi , lakini kwa wale watakaohudhuria show inayofata wataingia bure.