manyaki-1.jpg ...      ...

KAULI ZA MAKAO MAKUU JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KULA RUSHWA WALIZOPEWA NA PAUL MAKONDA

Kaimu DCI Boaz
Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kudai mbele ya Waziri Mkuu kuwa Wafanyabiashara wa Shisha walitaka kumhonga ili asiliongelee suala hilo lakini bado biashara hiyo ikaendelea na kumfanya ahisi kuwa Kamanda Sirro amepokea rushwa na kuwaruhusu waendelee kufanya biashara ya Shisha.
Leo November 18, 2016 Jeshi la Polisi Makao Makuu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Robert Boaz ametoa taarifa juu ya suala hilo. Kaimu DCI Robert amesema kuwa wamelipokea suala hilo na wameviachia vyombo husika vinavyohusika na masuala ya rushwa.
ALICHOKISEMA Kaimu DCI Boaz
“Jeshi la Polisi limepokea taarifa za tuhuma hizo na kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi inapotokea kiongozi yeyote wa Jeshi hilo amepatwa na tuhuma ni lazima achunguzwe ili kubaini ukweli, Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi juu ya tuhuma hizo.”



Previous
Next Post »