Star mmiliki wa Ngoma inayofanya vizuri kwa sasa ‘Kajiandae’, Ommy Dompoz, amefunguka na kudai kuwa tangu awe karibu na Mahasimu wawili Ali Kiba pamoja na Diamond Platnumz hakuna aliyewahi kutamka kuwa na tatizo na mwenzie.
Diamond, Ommy Dimpoz na AliKiba
Akiongea na The Playlist ya Times Fm jumamosi iliyopita, Ommy amedai mashabiki na Mitandao ndio inakuza swala hilo.
Lakini si Diamond wala Ali aliyewahi kutamka kuwa na bifu na mwenzio.
“Kwa bahati nzuri Nimekaa nao wote hakuna aliyesema kwamba ana bifu na mwenzie.” alisema Ommy