Rais wa Marekani Barack Obama anaondoka Jumatatu kwa ziara ya mwisho iliyopangwa nje ya nchi ya utawala wake kama rais, na washauri wake wanatarajia kuwa uongozi wa rais mteule Donald Trump ndio litakuwa suala kuu la mazungumzo na viongozi wenzake.
Naibu mshauri wa usalama wa kitaifa Ben Rhodes, alisema ziara ya rais Obama itamfikisha Ugiriki, Ujerumani na Peru, ikiwa ni ishara ya umoja kwa mataifa washirika wakaribu na ni njia ya kuonyesha uungaji mkono kwa ulaya iliyo na nguvu, umoja na ushirikiano.
Hotuba pekee iliyopangwa ni huko Ugiriki jumatano atazungumzia kazi iliyobaki kupambana na changamoto za kiuchumi nchini humo na maeneo mengine duniani wakati akiunga mkono ukuaji wa pamoja na kupambana na kutokuwa na usawa.
Rhodes pia alisema pia Rais Obama atafanya mazungumzo na waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsiparis kuonyesha uungaji mkono kwa kile watu wa Ugiriki walichopitia kutokana na majibu juu ya hali ya kiuchumi ambayo ilipelekea kunusuriwa kiuchumi na mataifa mengine na masharti magumu ya kukata matumizi na huduma za umma.
Vilevile anatarajiwa kufanya mazungumzo na kansela Angela Merkel wa Ujerumani hapo alhamisi.
Viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Italy na Hispania pia wanatarajiwa kuwepo katika mikutano mjini Berlin hapo ijumaa na wanatarajiwa kujadili masuala kuhusu vita vinavyoendelea dhidi ya kundi la Islamic State, masuala kuhusiana na uhamiaji, suala la Ukraine na uchaguzi ulIomalizika wa Marekani.