habari toka kwa mmoja wa watoto wa familia bwana ben sitta ambaye pia ni meya wa kinodoni amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake.
habari zinasema kuwa mh Sitta alikuwa amelazwa katika hospitali nchini ujerumani toka mwezi jana alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tenzi dume,ambapo inasemekana kuwa ugonjwa huo ulikuwa umeshamuathiri sehemu kubwa ya viungo vya mwili wake ikiwemo miguu na kumkwamisha kutembea.
watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wameendelea kutuma salamu za rambirambi kwa spika wa bunge wa sasa ndugu job ndugai na kwa familia akiwemo rais magufuli.