manyaki-1.jpg ...      ...

WAMAREKANI WATAIWAKILISHA DUNIA KUTETEA HAKI ZAO JUMANNE 8 NOV 2016-OBAMA

Rais wa Marekani Barack Obama ametahadharisha kwamba wapiga kura nchini Marekani watakuwa wakiamua kuhusu hatima ya Marekani kama taifa na ulimwengu kwa jumla watakapokuwa wanapiga kura Jumanne.
Ametoa wito kwa wafuasi wa chama cha Democratic wa asili zote kujitokeza kwa wingi na kumpigia kura Bi Hillary Clinton.
Amesema mpinzani wa Bi Clinton, Donald Trump wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kiraia ambazo watu wamezipigania kwa miaka mingi.
Rais Obama alikuwa anahutubu katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Carolina Kaskazini.
Lakini Bw Trump amesema Bw Obama anafaa kuacha kumfanyia kampeni Bi Clinton na badala yake aangazie kuongoza nchi.
"Ukweli ni kwamba, hakuna anayetaka miaka mingine minne ya Obama," ameambia wafuasi Pensacola, Florida.
Amesema sifa halisi za Bi Clinton zimedhihiriska siku za karibuni.
"Hatima ya jamhuri yetu imo kwenye mabega yengu," Rais Obama ameambia wafuasi wa chama cha Democratic katika jimbo linaloshindaniwa la Carolina Kaskazini.
"Hatima ya dunia imo hatarini nanyi pia, Carolina Kaskazini, tutahakikisha kwamba tunaielekeza katika njia ifaayo.
"Simo kwenye karatasi za kura, lakini nawaambia - usawa umo kwenye karatasi za kura, maadili yanapigiwa kura, haki imo kwenye kura, ufanisi umo kwenye karatasi za kura; demokrasia yetu imo kwenye kura."
Kampeni ya Bi Clinton imetikiswa na tangazo la mkuu wa FBI James Comey kwamba kuna barua pepe mpya kuhusu mgombea huyo zinazochunguzwa.
comey na hillary clinton
Bw Comey ameshutumiwa vikali kwa kutangaza habari hizo siku 11 kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Awali, Bw Obama alimkosoa hadharani kwa kuanzisha tena uchunguzi na kusema katika utamaduni wa Marekani, hatua huwa hazichukuliwi kwa kutegemea "maelezo ambayo hayajakamilika."
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Bw Obama kuzungumza hadharani tangu Bw Comey atangaze Ijumaa kwamba FBI wamepata barua pepe mpya ambazo huenda ziwe zinahusiana au huenda zisiwe zinahusiana na uchunguzi wa awali ambao ulikuwa umefanywa dhidi ya Bi Clinton.
Bi Clinton alikuwa ametuhumiwa kutumia sava ya barua pepe ya kibinafsi kufanya shughuli rasmi za serikali jambo ambalo baadhi wanasema lilihatarisha usalama wa taifa.

Barua pepe hizo mpya zilipatikana kwenye uchunguzi dhidi ya mbunge wa zamani Anthony Weiner anayetuhumiwa kumtumia msichana wa miaka 15 ujumbe wa kimapenzi jimbo la Carolina Kaskazini.
Bw Weiner ni mumewe mmoja wa wasaidizi wakuu wa Bi Clinton, Huma Abedin.
Hillary alipokutana na wafuasi wake  mgahawani

Previous
Next Post »