manyaki-1.jpg ...      ...

WANANCHI WA SUDANI WAISHIO MAREKANI WAANDAMANA


Matairi yakichomwa wakati wa maandamano Khartoum, Sudan. Majeshi ya usalama yalitumia gesi ya machozi kuvunja maandamano dhidi ya serikali.
Matairi yakichomwa wakati wa maandamano Khartoum, Sudan. Majeshi ya usalama yalitumia gesi ya machozi kuvunja maandamano dhidi ya serikali.
Wamarekani takriban 100 wenye asili ya Sudan walikusanyika nje ya ubalozi wa Sudan mjini Washington DC, katika maandamano ambayo wanasema wanataka yadumu mapambano ya raia wa Sudan.
Utawala wa rais Omar Al- Bashir hivi karibuni uliondoa ruzuku kwa mafuta na gesi na kuongeza bei ya umeme ili kujaribu kukabiliana na mfumuko mkubwa wa bei, lakini hivi sasa maelfu ya wasudan hawana uwezo wa kumudu mahitaji ya msingi.
Mwanaharakati Duha Elmardi yuko katika mshikamano na watu wa Sudan ambao wanataka mabadiliko ya kisiasa nchini kwao.
Elmardi amesema watu wa Sudan wameona hali ikiwa hivyo hivyo tangu mwaka 1989 na miaka ikienda huku wakipitia ubakaji na mateso. na kuongezea anadhani sasa watu wako tayari kupaza sauti zao.
“Upinzani wa kiraia,” amesema Elmardi, “umeandaliwa na vijana wa Sudan waliochoshwa na hali hiyo, hivyo kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kuandaa upinzani huo”.
Ongezeko la bei linawaumiza na hata kuwaua wasudan maskini kwa mujibu wa Khalid Tigani mwanachama muanzilishi wa Sudanese National Movement for Changes.
Anasema Sudan imekuwa katika matatizo yale yale ya kiuchumi tangu uhuru wa Sudan Kusini mwaka 2011, kwahiyo serikali kila wakati imekuwa ikiongeza bei za bidhaa ili kusuluhisha matatizo. Lakini kwa mujibu wa Benki ya Dunia, karibu nusu ya watu nchini Sudan wako katika hali ya umaskini hivyo hawawezi kumudu ongezeko la bei, ameongezea Tigani.
Previous
Next Post »