Shughuli ya kufunga mirija ya uzazi kwa wanaume (vasectomy) imetangazwa moja kwa moja kutoka chumba cha upasuaji kutoka mjini Nairobi, Kenya kama njia ya kuhamasisha watu kuhusu njia hiyo ya kupanga uzazi .
Takriban wanaume 150 walijiandisha kufanyiwa shughuli hiyo iliyochukua muda wa takriban dakika 20.
Madaktari walifanya shughugli hiyo nyuma ya jukwaa lilifunikwa katik ukumbi wa sanaa mjini Nairobi.
Wamaume nchini Kenya ambao mara nyingi wana hofu ya kufanyiwa zoezi hilo la kupanga uzazi mara nyingi uhofia kunyanyapaliwa.
Wale wanaoendesha kampeni ya zoeizi hilo wanasema kuwa ndiyo njia salama ya kupanga uzazi.
"Wanaume wengi hudhani kuwa zoezi hilo humnadili mwananamme kuwa mwanamke," Jack Zhang ambaye ni daktari kutoka Canada aliiambia BBC.
Baadhi ya wanaume wana hofu kuwa watu hufa kwa wingi barani Afrika kwa hivyo kuna haja ya kuzaa watoto wengi.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi, anasema kuwa baadhi ya wanaume walishiriki zoezi hilo baada ya kuchochewa na gharama ya kulea familia kubwa.
"Mbinu ambazo mke wangu alikuwa akitumia kupanga uzazi, zilikuwa na madhara kwake, kwa hivyo mimi niliamua kwenda kukatwa mirija ya ya uzazi," mwanamme moja aliiambia BBC.