Siku moja baada ya kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara kuripotiwa kwamba kimesitisha uzalishaji, watu mbalimbali wakiwemo wachumi, wanasiasa walitoa maoni tofautiofauti huku maneno mengi yakiendelea kwenye mitandao ya kiijamii.
Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage na ameeleza sababu za kiwanda hicho kufungwa na kuhusu maneno yaliyoenea kuwa wenye viwanda vya saruji wamefunga viwanda kugomea makaa ya mawe ya hapa nchini kwa madai kuwa hayana ubora kama wanayopata nje ya nchi.
.