manyaki-1.jpg ...      ...

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,UKAWA NGOMA NZITO.

Ikiwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache dunia zinazofanya uchaguzi wa amani na haki,na huku imebakia miezi kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka na huu utakaofanyika october kwa nchi nzima na kumpata rais wa tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania,wabunge wa majimbo husika na madiwani,
Muunganiko wa umoja wa katiba tanzania  (UKAWA) Unaowania kushika Dola ya nchi hivi majuzi imeshindwa kufikia muaafaka katika  mkutano wao na kuvunjika hivi majuzi,baada ya chama kishiriki cha  NCCR-MAGEUZI Kususia mkutano huo uliofanyika makao makuu ya chama cha wananchi CUF.
chanzo kinadai kuwa chama hicho kimepewa majimbo machache ya kuweka wagombea wao,ambao wao kama ukawa walikubaliana kuachiana baadhi ya majimbo kwa nia au malengo ya kukipiku chama tawala cha mapinduzi CCM.
Hofu na mashaka imeanza kuingia kwa wananchi baada ya taarifa hizo kuzagaa katika vyombo mbalimbali vya habari,ambavyo wanasema kuwa yawezekana yale maneno ya mgombea wa kigoma  kaskazini kupitia ACT Rugemara kabwe Zitto Zuberi yakawa ya Kweli ambavyo hivi majuzi alienguliwa toka chama cha CHADEMA Na kusema kuwa hayuko tayari kujiunga na chama hicho kwani viongozio wake wanagombea madaraka ivyo hata kama watapata nafasi ya kushika dola serikali yao itakuwa ya malumbano kila siku.


Previous
Next Post »