WAGENI WAALIKWA
FAMILIA YA RAIS
KAZI YA USANII
RAIS AKIKAGUA GWALIDE
WAANDISHI WA HABARI KAZINI
WASANII WAKITUMBUIZA
WAGENI WAALIKWA WAKIMIMINIKA UWANJANI KATIKA SHEREHE HIZO.
Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari ameapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo.
Viongozi kutoka mataifa mengi duniani wakiongozwa na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John kerry , rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma miongoni mwa wengine wengi.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?