Blatter anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Hussein kutoka Jordan
Wajumbe wa FIFA walioko nchini
Uswizi wameanza kumpigia kura rais mpya wa shirikisho hilo la soka
duniani huku shirikisho hilo likikabiliwa na shutuma za ufisadi.
Rais
wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter, ambaye ameongoza
shirikisho hilo kwa miaka 17 amewataka wajumbe wa mkutano mkuu kuunga
mkono nia yake ya kuchaguliwa tena kuongoza shirikisho hilo .
Akifungua
mkutano mkuu wa FIFA mjini Zurich, Bwana Mr Blatter alibainisha kuwa
shirikisho hilo linakabiliwa na matatizo - lakini akatoa wito kwa
wajumbe kushughulikia matatizo hayo kwa pamoja
Lakini kabla
upigaji kura , mpinzani mkuu wa bwana Blatter , Ali Bin al Hussein
mwanamfale wa Jordan, aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kumuunga mkono --
kwa ajili ya kuboresha mchezo wa soka
Siku ya pili ya Kongamano hilo ndio inayomchagua Rais wa FIFA.
Awali kumekuwa shinikizo kwa FIFA kuhairisha kongamano hili na pia uchaguzi wa urais.
hata
hivyo maombi hayo yalifutiliwa mbali na inatarajiwa kuwa rais Sepp
Blatter ataendelea mbele na uchaguzi ambao anakabiliana na mpinzani wake
mkuu mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan.
Blatter amesema kuwa tuhuma zinazoenea sasa ni njama dhidi ya FIFA
Blatter alifungua kongamano hilo kwa kuomba kuweko na umoja miongoni mwa maafisa wa FIFA.
Amesema kuwa tuhuma hizo ni njama ya kuibua maswali dhidi ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022.
Blatter
aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya
mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake.
Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa
upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye
pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi
yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi
wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji
mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao
wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika
mataifa maskini.
FBI inachunguza uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010
Naye Prince Ali anauungwaji mkubwa kutoka mataifa ya bara Ulaya.
Wajumbe hao wawili watahitaji zaidi ya robo tatu ya kura zote ili kupata ushindi wa moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.
Hilo lisipofanyika, kutakuwa na mkondo wa pili wa upigaji kura, ambapo mshindi wa kura nyingi atatangazwa mshindi.
FIFA
imekabiliwa wimbi la tuhuma za ufisadi ulaji rushwa na ubadhirifu
mkubwa baada ya maafisa wake wakuu saba kukamatwa na polisi nchini
Uswisi ilikujibu mashtaka nchini Marekani.
Maafisa wa kijasusi
kutoka Marekani FBI wamependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa
maafisa 14 wa FIFA kwa kula mlungula wa takriban dola shilingi 150
katika kipindi cha miaka 20.
FBI inachunguza uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010