Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu jaribio la mapinduzi la jumatano iliyopita.
Rais
Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura
alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la
waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab.
Aliwaambia
wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu
kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda . Wapinzani wake wanashuku ni njama ya kuidhinisha makabiliano makali na waandamani hapo kesho
Hata hivyo mwaandishi wa BBC
aliyeko Bujumbura anasema kuwa Nkurunziza hakuzungumzia lolote kuhusu
hali ilivyo nchini Burundi wala tishio la mapinduzi dhidi yake.
Aliondoka ghafla akiwa mongoni mwa msafara uliolindwa kikamilifu.
Wapinzani
wake hata hivyo wanasema huenda hiyo ni njama ya rais Nkurunziza
kuidhinisha makabiliano makali dhidi ya wapinzani wake ambao tayari
wameagiza wafuasi wao kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuendelea na
maandamano ya kumtaka asiwanie kipindi cha tatu katika kura za urais
zitakazofanyika mwezi ujao.
Al Shabab wametishia kuishambulia Burundi kufuatia mchango wake katika majeshi ya AMISOM
Duru kutoka kwa afisi za
maswala ya usalama wanje katika serikali ya Marekani na vile vile
maswala ya ndani ya serikali ya Uingereza zimekariri tishio hilo la Al
Shaabab dhidi ya Burundi kufuatia mchango wake katika jeshi la umoja wa
Afrika Amisom huko Somalia.
Marekani tayari imeagiza raia wake
kuondoka nchini humo kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi mbali na
kuzorota kwa hali ya usalama.