![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgq9ogkDLfo0BuKmPVWQRfYY1VMxoEC6NQFA1ewcCEXO6I7noedYB5vTMDwBCQMC7qKr5m0QnMZqX_tNaZfngtQsz7yPbafDOZzjaA65caI7-XxAbhLwtX584i5dZ-cqNbk-b-aJAewYVke/s320/150517122716_nkurunziza_624x351_afp.jpg)
Wakimbizi
saba Raia wa Burundi wamepoteza maisha katika kipindi cha wiki moja
kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Kuhara eneo la Kagunga mjini Kigoma
magharibi mwa Tanzania.Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR
linashirikiana kwa karibu na serikali ya Tanzania kuzuia kuenea kwa
ugonjwa wa kuhara katika Kambi. Maelfu ya raia wa Burundi wanaotoroka
mzozo wa kisiasa nchini mwao wanaingia nchini Tanzania kupitia mji wa
Kigoma katika kijiji cha Kagunga kwa ajili ya kupatiwa hifadhi.