Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuendelea kumshikilia Jamil Mukulu
ambaye ni kiongozi wa waasi wa ADF wa Uganda. Mukulu anayekabiliwa na
tuhuma kadhaa ikiwemo mauaji amefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa kumrudisha Uganda ili akashtakiwe
rasmi huko. Kiongozi huyo na kundi lake la ADF wanadaiwa kuhusika na
uhalifu katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mahakama imempa hadi tarehe 22 mwezi huu kuwasilisha pingamizi lake au
la atarejeshwa Uganda. Mwandishi wetu Kulthum Maabad amezungumza na
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania, Diwani
Athuman kuhusu hatua hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)