Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni
mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Tundu Lissu akihutubia
umati mkubwa wa wakazi wa Jiji la Arusha katika viwanja vya Shule ya
Msingi Ngarenaro katika mkutano uliokuwa katika sura ya UKAWA kwa
kuwashirikisha NCCR Mageuzi.
Mkutano huo nusura uathiriwe na mvua kubwa iliyonyesha wakati Mbunge wa
Kigoma Kusini Mh David Kafulila lakini mapenzi ya wafuasi wa CHADEMA kwa
chama na viongozi wao yaliwafanya wavumilie kunyeshewa mpaka mwisho.
Viongozi walikataa kukingwa na mvua hiyo na kujikuta wote wakilowa mwili
mzima kama wananchi wengine.
Katika hotuba yake, Mh Lissu aliwaeleza wakazi wa Arusha kitendo cha
Serikali ya CCM imeshakorofishana na karibu kila kundi la jamii kwa
kutaja wafanyabiashara, walimu, madaktari, madereva, wafanyakazi n.k ni
ishara kuwa chama hicho kimechokwa na kinaweza kuondoka madarakani
katika Uchaguzi wa mwaka huu ambao alisisitiza ni lazima ufanyike.
Waheshimiwa Kafulila na Lissu wakipokelewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Kalist Lazaro mwenye tisheti)
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), Mh David Kafulila ambaye kwa siku za karibuni amejizolea sifa lukuki kwa kuweza kuanzisha sakata la ESCROW na kulisimamia mpaka mwisho bila kuhofia vitisho mbalimbali. Katika mkutano huo Kafulila aliwashukuru wakazi wa Arusha kwa mapokezi mazuri na kusisitiza kuwa anajisikia furaha sana kuhutubia umati mkubwa Jijini hapa ambapo ni mji wa kihistoria katika harakati nyingi za kisiasa nchini. Kafulila aliwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba wawe na imani kupitia UKAWA na kwa kura zao wataweza kuitoa CCM madarakani.
Ukawa wakiimba wimbo wa taifa kabla ya mkutano kuanza