manyaki-1.jpg ...      ...

Uhamiaji:Ripoti kuhusu wahamiaji 4

Maelfu ya wahamiaji haramu wameripotiwa kuhama makwao barani Afrika na pia Mashariki ya Kati na kuhamia bara Ulaya kila mwaka.

Wengi wao wameabiri mashua ndogo za walanguzi wa watu na kufunga safari ya kuelekea bara ulaya kupitia bahari ya Mediterrenia.
Zaidi ya 1800 wamepoteza maisha yao wakijaribu kuvuka bahari hiyo ilikufuata ndoto ya maisha mazuri barani ulaya tangu mwaka huu uanze.
Idadi hii ya wafu ni mara 2o zaidi ya idadi ya wahamiaji haramu waliokufa maji mwaka uliopita.
BBC imewafuata wahamiaji wanne na hii hapa mukhtasari wa safari ya kutafuta maisha mazuri nga'mbo.
Staf Mustapha kutoka Ghana
Staf Mustapha
Staf na vijana wenzake kutoka Ghana walipanga kusafiri hadi ulaya kutafuta maisha mapya.
Wengi wao walipoteza maisha yao jangwani kati ya Niger na Chad.
Staf anasema kuwa kundi lililowatangulia lililokuwa na walibya liliangamia.
''tuliwaona wakiangamia lakini hatungeweza kuwasaidia maanake ilikuwa hatari mno''
''mmoja wenu akikosa chakula inakuwa vigumu sana kumgawia kwa sababu nawewe hujui kesho itakuwaje''Alisema Staf.
Safari yao ilianza mwaka wa 2013.
''Wakati mwengine kwasababu ya ukosefu wa vifaa maalum vya kubaini mwendo na kasi ya upepo tulikumbwa na hofu sana kwa sababu mawimbi hayakuwa mepesi''
Baada ya kufika Ugiriki, Staf alifululiza hadi Macedonia, hata hivyo alikamatwa na magenge haramu ya walanguzi wa madawa ya kulevya.
Magenge hayo sasa yanalazima awalipe iliwamuachilia huru.
Latifah na Ahmed kutoka Syria
Latifah na Ahmed
Latifah na Ahmed
Latifah, na mumewe Ahmed wakiambatana na watoto wao, Karim, 12, Hamza, 7, na Adam 2, walitoroka mapigano yaliyochacha nchini Syria mwezi Aprili mwaka huu.
Familia hii changa ilikuwa ikikusudia kutafuta mwanzo mapya ulaya katika taifa lenye uhuru na amani.
Familia hiyo iliyowasili Ujerumani ingali haijapata makao rasmi.
Safari yao ilianzia katika njia za chini kwa chini ilikuepuka makombora ya wapiganaji na majeshi ya serikali.
Latifa anasema kuwa pindi walipoabiri mashua hiyo iliyoundwa kwa mpira alikuwa na hakika kuwa wangezama majini.
Mtumbwi wenyewe waliokuwa nao ulikuwa takriban mita 6 pekee huku abiria wakiwa ni 40 pamoja na mizizgo yao.
Walilazimika kuwapigia askari wa majini kuomba msaada baada ya mtumbwi wao kukabiliwa na mawimbi makali katika bahari ya Ugiriki.
''amini usiamini tulilazimika kutupa mizigo yetu baharini na mawimbi yalipozidi tukajitosa ndani ya bahari angalau kunusuru nafsi yetu''
''Hatimaye askari wa kushika doria baharini kutoka Uturuki na wale wa Ugiriki walituokoa.
Latifa anasema walikuwa ''wanahisi baridi kali na njaa''
Maafisa wa uturuki waliwapeleka ufukweni lakini siko walikotaka kwenda.
Iliwabidi kupanga safari nyingine sasa iliyowapeleka hadi Ugiriki.
''Tulipofika katika mji mkuu wa Athens' tulijitahidi na kwenda Macedonia tukavuka Serbia ndipo tukawasili hapa Ujerumani.'' anasema Latifah.
Om Motasem alitoroka Syria vita vilipoibuka.
Om Motasem
Om Motasem alitoroka Syria vita vilipoibuka.
wakati huo alikuwa akiishi pamoja na mume wake, Abu Nimr, 42,mke mwenza na watoto wao 15.
Isitoshe waliishi na mavyaa wake katika mji mkuu wa Damascus.
Ilikuwa ni maisha aliyoridhika nayo hadi pale zilipozuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mnamo mwezi Julai 2013 Abu Nimr na Om Motasem walitorokea usalam wao mjini Alexandria nchini Misri.
Wakiwa ugenini maisha yalibadilika mno na ndipo wakagundua kuwa wao ni wakimbizi.
Kifungua mimba wake aliondoka na kukimbilia bara ulaya kutafuta mwanzo mpya.
Safari ya maisha yake yalimfikisha mjini Berne Ujerumani.
Om Motasem aliamua kumfuata huko akiandamana na watoto wake wawili wakike mmoja mwenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye umri wa miaka 16.
Watatu hao walistahimili mawimbi makali na baridi katika safari yao ya siku tatu kuvuka bahari ya Mediterrania hadi kwenye kisiwa cha Lampedusa.
''tulifunga safari usiku wa manane mle kwenye mashua mlikuwa na wanawake na watoto
Omar Gassama kutoka Senegal
Omar Gassama,18: Gambia-Italia
Tineja Omar Gassama, mwenye asili ya Senegal alisomea nchini gambia Gambia, hatimaye amewasili mjini Turin Kaskazini mwa Italia.
Alikwenda Libya kutafuta ajira wakati huo akiwa na umri wa miaka 16.
Alitatizika mno kupata kazi kutokana na hali yake ya uhamiaji haramu.
Nchini Libya alibaguliwa kwa misingi ya rangi yake na akalazimika kutafuta suluhu moja ikiwa ni kwake kumlipa mlanguzi wa binadamu iliamuondoe nchini humo.
Mlanguzi huyo alimpelekea mjini Sicily Italia mwezi Aprili mwaka uliopita.
''bahari ilikuwa ya kutisha mno'' anaelezea.
Siku mbili tu baada ya kung'oa nanga wahamiaji wenza waliokolewa na boti la wanamaji kutoka Italia.
Walipelekwa katika hoteli moja ambako alikutana na wahamiaji wengine wengi wao wakiwa wenye asili ya Kiafrika yaani Nigeria , Somalia na Eritrea.
Walipewa chakula na mavazi pamoja na kiinua mgongo.
Omar hivi sasa amehamia Turin Italia ambako anaishi kwa pamoja na wahamiaji wenza kutoka Senegal.
Omar tayari ameanza kujifunza Kiitaliano huku akisubiri uamuzi kuhusu ombi lake la kutafuta kutambuliwa kama mhamiaji.
Anasema kuwa huenda akahamia Ujerumani ama Uingereza katika siku za usoni.
Previous
Next Post »