Bibi
kizee akiwa amejifunga skafu yenye maneno “Mabadiliko” wakati mgombea kiti cha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, akiwakilisha vuguvugu
la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, Mh. Edward Lowassa, al;ipohutubia
mkutano wa kampeni mjini Iringa leo Jumapili Agosti 30, 2015. Huu ni mkutano wa
kwanza tangu azindue kampeni Agosti 29, 2015 pale Jangwani ambapo maelfu ya
wananchi walihudhuria
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, akimnadi Mh. Lowassa mjini Iringa leo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania
katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William
Joseph Mungai, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015
Umati wa watu mjini Iringa kwenye mkutano wa kampeni wa UKAWA uliohutubiwa na Mh. Lowassa
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania
katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa wakati wa Mkutano wa
Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mkoani Iringa leo Agosti 30,
2015
Mh. Lowassa akihutubia wananchi kwenye mkutanoi wa kampeni mjini Iringa leo
Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa |