Mji muhimu wa mwisho uliokuwa mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini
magharibi mwa Somalia wa Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya
Muungano wa Afrika (AU) -miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi
kali kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo
wamesema vikosi vya Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi
wa mashambulizi ya anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al
Shabaab waliutoroka usiku.Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya jeshi la Somalia, vilifanikiwa kuuteka mji huo baada ya mashambulizi makali. Majeshi kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.
Wakazi wanasema kamanda mmoja wa Somali na vyombo vya habari vinavyounga mkono Al Shabaab wamethibitisha kuchukuliwa kwa mji huo.
Kundi la Al shaabab lina uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda linapigana dhidi ya serikali ya Somalia kwa ajili ya udhibiti wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mashambulizi ya ndege zisizokua na rubani (drone) zilizoshambulia ziliripotiwa kuwauwa makamanda wa ngazi ya juu wa Al Shabaab.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika sasa wanaudhiobiti mji wa Baardheere uliokuwa mikononi mwa Alshaabab-Somalia
Wanajeshi wa AU waliuteka mji wa Baardheere baada ya Alshaab kuukimbia
Wanajeshi wa serikali ya Somali pia walishiriki kuwaondosha nje ya mji wa Baardheere Al shaabab
http://frankmanyaki.blogspot.com/