Barack Obama
Katika
mahojiano maaluma na BBC , Rais wa Marekani Barack Obama amesema
kushindwa kudhibiti silaha nchini mwake ni jambo lililomsononesha katika
utawala wake.
Amesema Marekani ni nchi pekee iliyoendelea ambayo
haina sheria ya kutosha kuhusu usalama wa silaha, hata wakati huu ambapo
kumekuwa na marudio ya matukio ya mauaji.Obama amesema magaidi wameua chini ya wamarekani mia moja tangu shambulio la kigaidi la Septemba 11, lakini waliouawa kwa matukio ya kutumia silaha ni makumi kwa maelfu katika kipindi hicho.
Rais Obama alijaribu kusukuma mbele sheria ya udhibiti wa silaha baada ya tukio la mauaji kwenye shule moja inayojulikana kwa jina la Sandy Hook School mwaka 2012, lakini sheria hiyo ya kubana matumizi ya silaha ilikataliwa na bunge la Congress.http://frankmanyaki.blogspot.com/