manyaki-1.jpg ...      ...

DIAMOND PLATINUMZ ATAMANI PESA NDEFU YA MAALI KWA TIFFA TOKA KWA MTOTO WA ALIKIBA


Mapema Leo  November 22, 2016 hipo stori kuhusu picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha watoto wa mastaa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz na Alikiba huku ikiwa imeandikwa (Natamani mkikua mje kuoana ili baba zenu wapatane).

Kwa mujibu wa Soudy Brown baada ya kuzagaa kwa picha hiyo, kuna tajiri fulani jijini Dar es salaam ambaye inadaiwa ni shabiki wa wasanii hao, amejitokeza na kusema yuko tayari kumlipia mahari mtoto wa Alikiba ili aje kumuoa Tiffa, mtoto wa Diamond.
Soudy Brown amezungumza na Diamond Platnumz kuhusu suala hilo na je ana maamuzi gani juu ya mwanaye kutolewa mahari.
“Ntampiga hela zake hatokaa aamini, sijajua ntataka walipe kiasi ila sitatoa bure uislamu huo sina mimi, eti sijui uje tu na kitabu aaah wapi, hapa hela tu tena itakua hela nyingi sana labda itokee mwenyewe atunuku ila kama atanisikiliza mimi baba yake atapiga hela nyingi  tu hata Dola milioni 1 ndogo” – Diamond
Sikiliza sehemu ya mahojiano hayo.

Previous
Next Post »