manyaki-1.jpg ...      ...

Kanye west akatwa pesa kwa kukatisha show yake gafla.

Kanye West amekuwa kwenye headlines mbali mbali wiki hii, na mojawapo ni hii ya kukatisha show aliyokuwa akiifanya huko Sacramentino California na kuanza kuwachana Beyonce na Jay Z kwenye steji kwa alichodai kwamba wamemkosea.
Baada ya kumaliza kuwachana Jigga na Bey Kanye alitupa Mic chini na kuondoka, kitu ambacho kililalamikiwa na mashabiki kwa sababu alikuwa ameperfom nyimbo tatu tu.
Waandaaji wa show hiyo  wamewaahidi mashabiki kulipwa pesa zao ndani ya siku 5 mpaka 7 za kazi , lakini  kwa wale watakaohudhuria show inayofata wataingia bure.
Hata hivyo Kanye West ameahirisha show hiyo ambayo ni moja kati ya show zake kwenye tour yake ya Saint Pablo baada ya kuugua ghafla na kulazwa Hospitali Jumatatu ya November 22, 2016 na kwa mujibu wa ripoti za kidaktari zinasema Kanye anasumbuliwa na msongo wa mawazo pamoja na uchovu.
Previous
Next Post »