manyaki-1.jpg ...      ...

MISRI YAGUNDUA MJI WENYE ZAIDI YA MIAKA 5,000




Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 5,000 iliyopita.
Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa.
Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos.
Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo.
Inaaminika kwamba mji huo ulikuwa makao ya maafisa wakuu wa se
rikali na wachimbaji na wajenzi wa makaburi, ambao ulifana enzi za kwanza kabisa za Misri ya kale.
Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.
Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na mawe.
Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa.
Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji makuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.

Previous
Next Post »